KICC JUKWAA LA KUKUTANISHA WADAU WA AFYA KATIKA MAONYESO YA TECKONOLOJIA MBALIMBALI
Mwandishi: Caleb Omwama
Kenyatta International Conference Centre (KICC), imetumika kuonyesha njisi inavyoweza kuwa jukwaa la kuunganisha afya,teknolojia na biashara. Hii ni dhihirisho kuwa KICC ni Zaidi ya ukumbi wa mikutano, hasa wataalamu katika fani mbalimbali za afya walipoweza kujumuika kwa lengo la kuonyesha hatua ambazo taifa la kenya limeweza kupiga katika sekta ya afya.
Uwanja huu uliweza kuwapa fursa wakenya na wageni kwa ujumla kupata ufahamu kuhusu mbinu za kisasasa za matibabu kupitia hafla ya Health Summit 2026.
Maarifa yameweza kukutanisha wataalamu wa afya, watafiti, serikali, wafanyabiashara, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Tiba Cha Kenya (KMTC) na wananchi, haya yalidhihirisha kuwa ufahamu ni nguvu, kauli inayoweza kubadilisha maisha ya wengi kutokana na kuelimika, na uelewa wa huduma bora za afya.
Vifaa vya kisasa vya kitabibu vinaonyesha njisi afya teknolojia, ubunifu, huduma bora inaweza kuleta suluhisho kwa changamoto tofautitofauti za kiafya.
Hafla hii imeweza kuleta ufahamu kuhusu:
- Teknolojia mpya za uchunguzi na matibabu, ikiwemo vifaa vya kisasa vya hospitali.
- Mbinu za kuzuia magonjwa mbalimbali, hasa magonjwa hatari ambukizi na umuhimu wa uchunguzi wa mapema.
- Njia bora za kujikinga na magonjwa kupitia elimu ya afya.
- Bidhaa na huduma mpya za afya zinazopatikana nchini.
- Ushirikiano kati ya wataalamu, serikali, taasisi na sekta binafsi katika kuuboresha afya vya wananchi.
Vilevile, viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa jamuhuri ya kenya, Dkt.Wiliam Samoei Ruto, pamoja na waziri wa afya, Mhe.Aden Duale, waliuungana na wataalamu na wadau mbalimbali katika Kenya Health Summit 2026 ilioyofanyika KICC.
Waziri Duale alisisitiza umuhimu wa wakenya kujisajili katika SHA ili kupata fursa ya huduma za afya. Rais wa kenya kwa upande wake aliweza, kueleza maendeleo yaliyopatikana kupitia SHA na kusisitiza umuhimu wa mifumo ya kidijitali katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.
Hakika KICC ni mahali ambapo pamewakutanisha wataalamu na wote wenye mawazo mapya na maono. Kupitia fursa ya kuandaa Health summit 2026, KICC imeendelea kudhihirisha nafasi yake kama kitovu cha mikutano na matukio yenye mchango maendeleo ya taifa na kuvuka mipaka.
Picha za matukio mbalimbali katika maonyesho ya Health Summit 2026.

Courtyard inaweza kutumika kwa matukio makubwa ya nje , ikiwemo maonyesho, uzinduzi wa bidhaa, hafla za kampuni, burudani na tamasha.Eneo hilo linaweza kuhudumia takriban watu 6,000.



