Mabango yanaonyesha uwepo wa taasisi, kampuni na mashirika yanayohusika na huduma za afya na teknolojia katika eneo la courtyard KICC lililopo upande wa city way.
Courtyard inaweza kutumika kwa matukio makubwa ya nje , ikiwemo maonyesho, uzinduzi wa bidhaa, hafla za kampuni, burudani na tamasha.Eneo hilo linaweza kuhudumia takriban watu 6,000.
