KICC JUKWAA LA KUKUTANISHA WADAU WA AFYA KATIKA MAONYESO YA TECKONOLOJIA MBALIMBALI

KICC JUKWAA LA KUKUTANISHA WADAU WA AFYA KATIKA MAONYESO YA TECKONOLOJIA MBALIMBALI

Mwandishi: Caleb Omwama

Kenyatta International Conference Centre (KICC), imetumika kuonyesha njisi inavyoweza kuwa jukwaa la kuunganisha afya,teknolojia  na biashara. Hii ni dhihirisho kuwa KICC ni Zaidi ya ukumbi wa mikutano, hasa wataalamu  katika fani mbalimbali za afya walipoweza kujumuika kwa lengo la kuonyesha hatua ambazo taifa la kenya limeweza kupiga katika sekta ya afya.

Uwanja huu uliweza kuwapa fursa wakenya na wageni kwa ujumla kupata ufahamu kuhusu mbinu za kisasasa za matibabu kupitia hafla ya Health Summit 2026.

Maarifa yameweza  kukutanisha wataalamu wa afya, watafiti, serikali, wafanyabiashara, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Tiba Cha Kenya (KMTC) na wananchi, haya yalidhihirisha kuwa ufahamu ni nguvu, kauli inayoweza kubadilisha maisha ya wengi kutokana na kuelimika, na uelewa wa huduma bora za afya.

Vifaa vya kisasa vya kitabibu vinaonyesha njisi afya teknolojia, ubunifu, huduma bora inaweza kuleta suluhisho kwa changamoto tofautitofauti za kiafya.

Hafla hii imeweza kuleta ufahamu kuhusu:

  • Teknolojia mpya za uchunguzi na matibabu, ikiwemo vifaa vya kisasa vya hospitali.
  • Mbinu za kuzuia magonjwa mbalimbali, hasa magonjwa hatari ambukizi na umuhimu wa uchunguzi wa mapema.
  • Njia bora za kujikinga na magonjwa kupitia elimu ya afya.
  • Bidhaa na huduma mpya za afya zinazopatikana nchini.
  • Ushirikiano kati ya wataalamu, serikali, taasisi na sekta binafsi katika kuuboresha afya vya wananchi.

Vilevile, viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa jamuhuri ya kenya, Dkt.Wiliam Samoei Ruto, pamoja na waziri wa afya, Mhe.Aden Duale, waliuungana na wataalamu na wadau mbalimbali katika Kenya Health Summit 2026 ilioyofanyika KICC.

Waziri Duale alisisitiza umuhimu wa wakenya kujisajili katika SHA ili kupata fursa ya huduma za afya. Rais wa kenya kwa upande wake aliweza, kueleza maendeleo yaliyopatikana kupitia SHA na kusisitiza umuhimu wa mifumo ya kidijitali katika kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Hakika KICC ni mahali ambapo pamewakutanisha wataalamu na wote wenye mawazo mapya na maono. Kupitia fursa ya kuandaa Health summit 2026, KICC imeendelea kudhihirisha nafasi yake kama kitovu cha mikutano na matukio yenye mchango maendeleo ya taifa na kuvuka mipaka.

Picha za matukio mbalimbali katika maonyesho ya Health Summit 2026.  

Mabango yanaonyesha uwepo wa taasisi, kampuni na mashirika yanayohusika na huduma za afya na teknolojia katika eneo la courtyard KICC lililopo upande wa city way. Courtyard inaweza kutumika kwa matukio makubwa ya nje , ikiwemo maonyesho, uzinduzi wa bidhaa, hafla za kampuni, burudani na tamasha.Eneo hilo linaweza kuhudumia takriban watu 6,000.
Mabango yanaonyesha uwepo wa taasisi, kampuni na mashirika yanayohusika na huduma za afya na teknolojia katika eneo la courtyard KICC lililopo upande wa city way.
Courtyard inaweza kutumika kwa matukio makubwa ya nje , ikiwemo maonyesho, uzinduzi wa bidhaa, hafla za kampuni, burudani na tamasha.Eneo hilo linaweza kuhudumia takriban watu 6,000.
Ndani ya hema kubwa lilioko katika eneo la courtyard kuna mabanda madogomadogo yanaonyesha nembo za hospitali, bidhaa mbalimbali na mashine za kisasa zinazohusiana na teknolojia za afya.
Ndani ya hema kubwa lilioko katika eneo la courtyard kuna mabanda madogomadogo yanaonyesha nembo za hospitali, bidhaa mbalimbali na mashine za kisasa zinazohusiana na teknolojia za afya.
Picha yaonyesha aina ya maabara inayotembea( Bionear Mobile Laboratory) katika eneo la courtyard ndani ya KICC. Maabara hii yenye teknolojia ya hali ya juu inatumika kupima magonjwa hatari ambukizi kama vile Ebola,Virusi vya korona pamoja na magonjwa mengineo.
Picha yaonyesha aina ya maabara inayotembea( Bionear Mobile Laboratory) katika eneo la courtyard ndani ya KICC. Maabara hii yenye teknolojia ya hali ya juu inatumika kupima magonjwa hatari ambukizi kama vile Ebola,Virusi vya korona pamoja na magonjwa mengineo.
Banda kuu lilioko katika viwanja vya COMESA, KICC Nairobi, eneo hili lilitumika na washirika mbalimbali katika idhara ya afya kuhutubia wananchi.
Banda kuu lilioko katika viwanja vya COMESA, KICC Nairobi, eneo hili lilitumika na washirika mbalimbali katika idhara ya afya kuhutubia wananchi.
Banda hili limetumika kwa uhamasishaji wa lishe bora na umuhimu wa kuzingatia virutubishi kwa kila vyakula tunavyotumia, vilevile kuelimisha umma kuhusu sumu ya aflotoksini.
Banda hili limetumika kwa uhamasishaji wa lishe bora na umuhimu wa kuzingatia virutubishi kwa kila vyakula tunavyotumia, vilevile kuelimisha umma kuhusu sumu ya aflotoksini.
Translate »
Scroll to Top
  • CPA Samuel Waweru Mwangi is the Chairperson of Kenyatta International Convention Centre. 
  • Prior to joining the Corporation, Mwangi has served as head of Finance in various Corporates. 
  • Mwangi is a seasoned finance professional with extensive experience in accounting, financial management, and operations.
  • He holds a Master of Science in Finance and Investment from and a Bachelor of Business Administration (Accounting and Finance) from KCA University. 
  • He is a certified Public Accountant and a certified Investment and Financial Analyst (CIFA). He is also a member of ICPAK
  • Mwangi boasts of a proven track record in overseeing financial operations, managing budgets, and conducting detailed financial analyses.
  • He is also a successful entrepreneur.
  • His vast expertise in financial performance and management coupled with his leadership skills will be instrumental in steering Kenya’s MICE sector to even greater
    heights.